Posts

Showing posts from June, 2020

TFF YARUHUSU MECHI ZA KIRAFIKI KWA MASHARTI

Image
Rais wa TFF Wallace Karia Siku moja baada ya kuzuia michezo ya kirafiki kwa timu za soka, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limeziruhusu timu kuendelea na mechi hizo huku likitaka zizingatie muongozo wa kujikinga na virusi vya Corona. Zuio hilo lilitangazwa jana jioni kufuatia kuonekana mashabiki wengi waliohudhuria mechi za kirafiki zilizohusisha timu za Simba, Yanga, Azam, KMC, Transit Camp, Namungo na Ndanda na hivyo kuvunja muongozo wa kujikinga na virusi vya Corona uliotolewa na Wizara ya Afya, TFF na Bodi ya Ligi. Rais wa TFF, Wallace Karia amesema baada ya kikao kilichoketi asubuhi, wamefikia muafaka na kuruhusu mechi za kirafiki ziendelee lakini kwa masharti ambayo ni lazima yatekelezwe.