TFF YARUHUSU MECHI ZA KIRAFIKI KWA MASHARTI
Siku moja baada ya kuzuia michezo ya kirafiki kwa
timu za soka, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo limeziruhusu timu kuendelea
na mechi hizo huku likitaka zizingatie muongozo wa kujikinga na virusi vya
Corona.
Zuio hilo lilitangazwa jana jioni kufuatia kuonekana
mashabiki wengi waliohudhuria mechi za kirafiki zilizohusisha timu za Simba,
Yanga, Azam, KMC, Transit Camp, Namungo na Ndanda na hivyo kuvunja muongozo wa
kujikinga na virusi vya Corona uliotolewa na Wizara ya Afya, TFF na Bodi ya
Ligi.
Rais wa TFF, Wallace Karia amesema baada ya kikao
kilichoketi asubuhi, wamefikia muafaka na kuruhusu mechi za kirafiki ziendelee
lakini kwa masharti ambayo ni lazima yatekelezwe.
Comments
Post a Comment