BANCE ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA
OUAGADOUGOU, Burkinafaso
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burkinafaso
Aristide Bance ,35, ametangaza rasmi kustaafu kucheza timu ya taifa baada ya
miaka 17 toka alipoanza kuichezea 2003.
Bance ambaye amecheza soka katika mataifa mbalimbali
ya Asia, Afrika na Ulaya sasa ataendelea kuitumikia timu yake ya Horoya AC ya
Guinea pekee.
Bance ameichezea Burkinafaso michezo 73 na kufunga
magoli 22, alikuwa sehemu ya kikosi cha Burkinafaso kilichoshiriki michuano ya
AFCON 2013, 2015 na 2017.
Mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ilikuwa Novemba
2017 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu
kucheza Kombe la Dunia 2018.
Comments
Post a Comment