DSJ YAPANIA KUTISHA MICHEZONI
Na Arone Mpanduka
NAIBU Waziri wa Michezo wa Chuo cha Uandishi wa Habari
Dar es Salaam(DSJ), Walter Masawe anaamini timu ya Chuo hicho itafanya maajabu katika
mashindano mbalimbali ya ndani na nje hasa mashindano yanayoshindanisha vyuo mbalimbali.
Walter ameyasema hayo chuoni hapo baada ya kuanza rasmi
maandalizi ya kuvisuka vikosi vipya vya Mpira
wa Miguu kwa wavulana pamoja na Mpira wa Pete kwa wasichana kwa ajili ya ushiriki
wa mashindano ya Vyuo Vikuu yanayo tarajiwa kuanza hivyi karibuni.
Amesema awali walikuwa wakishidwa kuwika kwenye mashindano mengi kutokana na ubora wa vikosi vya
wapinzani kwa kuwa wao walikuwa hawafanyi
mazoezi kama inavyotakiwa ndiyo maana walikuwa wakiboronga kwenye mechi
walizokuwa wanacheza.
“Hapo awali tulikuwa tunafugwa hovyo hovyo kwasababu
tulikuwa tunaenda kushiriki na sio kushindana, lakini kwa sasa tupo vizuri hasa
kwa hatua za awali kwani tumeshapata wachezaji wazuri na kadri siku zinavyokwenda
tutazidi kuwa vizuri zaidi na kupambana katika michezo mikubwa zaidi,”alisema
Walter.
Amesema, kwa sasa wamerudisha mchezo wa mpira wa pete
kwa kina dada, ambao ulisahaulika kwa muda kutokana na ukosefu wa vifaa vya mchezo
huo na kuwa na mwitikio mdogo kwa wasichana waliotakiwa kujitokeza kushiriki katika
mchezo huo
Amesema kuwa Kamati ya michezo imepokea maoni mbalimbali
kuhusiana na michezo mingine tofauti na Mpira wa Miguu na Pete na hivyo ameomba
wanafunzi kama wangependa michezo mingine
iongezwe, wanakaribishwa kujitokeza na kusema ni mchezo upi uongezwe ili wawe na
timu nyingi za mashindano.
“Sasa hivi tutakuwa na timu mbili pekee, timu ya Mpira
wa Miguu kwa wavulana na Mpira wa Pete kwa upande wa wasichana, na hapa kwa wasichana tunatengemea kufanya makubwa zaidi
,sasa hivi muitikio ni mkubwa, isipokuwa
kama kuna mtu anapenda kucheza michezo mingine tofauti na hii, tunamkaribisha
kutoa maoni yake kuhusu mchezo anaopenda uongezwe,” alisema Walter.
Comments
Post a Comment