LIGI KUU CHINA YAREJEA

Wachezaji wakishangilia goli katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya China

CHINA

Chama cha soka cha China kimetangaza ligi kuu nchini humo itaanza Julai 25,2020 baada ya kuchelewa kuanza kutokana na uwepo wa virusi vya Corona.

Chama hicho kimetangaza ligi hiyo itachezwa katika miji ya Dalian na Suzhou, ambapo timu 16 zitagawanywa kwenye makundi mawili.

Ligi hiyo ambayo Guangzhou ndio mabingwa watetezi, awali ilitarajiwa kuanza Februari 22, lakini ikaahirishws kwa sababu ya virusi vya Corona ambavyo vilianzia huko huko China

Comments