SIMBA YAIFUATA YANGA KOMBE LA FA




Wachezaji wa Simba na Azam FC wakimenyana kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la FA kwenye uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.


Na Arone Mpanduka,DAR ES SALAAM

Ushindi wa mabao 2-0 walioupata Simba leo Uwanja wa Taifa mbele ya Azam FC unaipa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali na itakutana na Yanga.

Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam FC wakionekana kuwa na shauku kubwa ya kupata ushindi ila mambo yalikuwa magumu kwa leo.

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco dakika ya 40 akimalizia pasi ya Francis Kahata kwa kichwa.

Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko ambapo Simba walikwenda vyumbani wakiwa vifua mbele kwa bao hilo moja.

Clatous Chama alirejea kambani dakika ya 56 kwa shuti kali ndani ya 18 akimalizia pasi ya Shomari Kapombe. 

Mpaka dakika 90 zinakamilika jitihada za Azam FC kupenya ngome ya Simba ziligonga mwamba.

Beki wa kulia Kapombe dakika za mwisho alibebwa kwenye machela baada ya kuchezewa faulo na Domayo.

Sasa ni rasmi, Yanga aliyetangulia kutinga hatua ya nusu fainali jana, Juni 30 kwa kumtungua Kagera Sugar mabao 2-1 anakutana na Simba.

Comments