UWANJA WA AL SHABAAB KUANZA KUTUMIKA
Mogadishu, SOMALIA
Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amefungua rasmi uwanja wa mpira wa Mogadishu wenye uwezo wa kubeba watu 35,000 ikiwa ni katika hatua za nchi hiyo kujijenga baada ya takribani miongo mitatu ya mapigano.
Uwanja huo ambao uliwahi kuchukuliwa na kundi la waasi la Al-Shabaab na baadae kuanza kutumika kama kambi ya vikosi vya jeshi la umoja wa Afrika AMISOM —ulifanyiwa marekebisho baada ya vikosi hivyo kuondoka mwishoni mwa mwaka 2018.
Umoja wa Ulaya, Norway na washirika wengine wa maendeleo walichangia utengenezaji upya wa uwanjani huo baada ya serikali kukabidhiwa na AMISOM Agosti 2018
AMISOM na Jeshi la Taifa la Somalia walifanikiwa kuuchukua uwanja huo kutoka kwa Al Shabaab Septemba 06, 2011.
Al Shabaab walikuwa wanautumia uwanja huo kama kituo chao cha shughuli za ugaidi.
Baada ya AMISOM kuuchukua uwanja huo wakawa wanautumia kama kambi ya
vikosi vyao, mpaka walipourudisha kwa serikali mwaka 2018 na kuanza
kufanyiwa marekebisho
Kwa miaka mingi sasa Somalia imekuwa ikicheza mechi zake za kimataifa nchini Djibouti kwa sababu ya hali mbaya ya kiusalama nchini kwao.
Comments
Post a Comment