WILLIAN HUYOO ARSENAL
London, ENGLAND
Arsenal imetajwa kuongoza mbio za kumuwania winga wa
Chelsea, Willian baada ya nyota huyo raia wa Brazil kushindwa kufikia
makubaliano ya kusaini mkataba mpya na klabu yake.
Taarifa iliyotolewa na mtandao wa The Sun, imefichua
kuwa mazungumzo baina ya wawakilishi wa Arsenal na wale wa mchezaji huo yako
katika hatua za mwisho ambapo Willian mwenye umri wa miaka 31 atajiunga nao
akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika msimu huu.
Chelsea ilikuwa inapanga kumuongezea mkataba wa
miaka mwili, nyota huyo huku yeye akihitaji uwe na urefu wa miaka mitatu jambo
ambalo wameshindwa kufikia muafaka na kupelekea Willian aamue rasmi kufungasha
virago na kusaka malisho mazuri zaidi.
Klabu takribani tano zimetajwa kuingia katika vita
ya kumuwania Willian lakini ni Arsenal ambayo kwa mujibu wa taarifa kutoka
katika vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wameshafikia muafaka na
kilichobakia ni mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu.
Comments
Post a Comment