MORRISON ASHINDA KESI

 

Winga wa Simba, Benard Morrison

Na Arone Mpanduka,  DAR ES SALAAM

KIUNGO wa Yanga, Bernard Morrison raia wa Ghana leo Agosti 12 ameshinda shauri lake dhidi ya Yanga ambalo lilikuwa ni kuhusu mkanganyiko wa mkataba wake ndani ya klabu hiyo.

Morrison alikuwa akisema kuwa mkataba wake ni wa miezi sita na umekwisha muda wake huku Yanga ikieleza kuwa alisaini dili lingine la miaka miwili.

Baada ya kesi hiyo kuskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo tangu, Agosti 10,11 na 12 leo shauri limetolewa rasmi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF).

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala, amesema mkataba wa Yanga na Morrison, una mapungufu makubwa upande wa Yanga na wamempa faida Morrison.

."Tumekuwa makini katika kufuata haki na kamati yetu ilikuwa makini, kulikuwa na mapungufu makubwa upande wa tarehe ambapo kuna sehemu ilionyesha kuwa amesaini Machi 20 na nyingine ikionyesha tarehe tofauti.

"Pia kuna ukurasa wa saini kwenye mkataba unaonyesha kuwa umekatwa jambo ambalo linaonyesha kwama kulikuwa kuna tatizo kwenye masuala ya mkataba ni mapungufu makubwa hivyo tunampa ushindi Morrison anakuwa huru kwa sasa.

"Kazi yetu tumemaliza ila Morrison anapelekwa kamati ya Maadili ya TFF kutokana na kosa la kusaini mkataba na timu nyingine (Simba), wakati kesi yake inaendelea kusikilizwa na kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji...

"Kesi hii inayokwenda kamati ya maadili, haina mahusiano na hii ya Yanga dhidi ya Morrison, ambayo yeye ameshinda na ni mchezaji huru. Mchezaji mwenyewe amekiri kuwa amefanya hivyo, ikiwa Yanga hawajaridhika na maamuzi haya ni ruksa kwenda kukata rufaa," amesema.

Comments