NYOTA MMOJA BARCELONA ANA CORONA
Kikosi cha timu ya soka ya Barcelona ya Hispania |
BARCELONA, Hispania
Barcelona imesema kuna mchezaji mmoja amebainika
kuwa na ugonjwa wa Covid 19.
Mchezaji huyo ambaye jina lake limefichwa, ni
miongoni mwa wachezaji 9 walioripoti katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya
na tayari amejiweka karantini nyumbani kwake huku akiwa hana dalili yoyote ya
kuumwa.
Barcelona imesema hajasogeleana na mchezaji yoyote
ambaye atasafiri kwenda Ureno kucheza mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya.
Tayari Valencia ilithibitisha visa viwili vya corona
wiki hii huku Atletico Madrid ikiripoti watu wawili kabla ya mechi ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Barcelona itakipiga na Bayern Munich Ijumaa katika
mechi ya robo fainali huku Atletico na RB Leipzig wakitangulia kesho.
Comments
Post a Comment