UKIMKOHOLEA MWENZIO TU, KADI

Wachezaji wakileteana ubabe uwanjani

LONDON, England

Wakati msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu chama cha soka nchini humo kimeandaa kanuni mpya ambayo itaanza kutumika katika msimu ujao.

Kanuni hiyo inaeleza kuwa ikiwa mchezaji wa timu moja atamkoholea mchezaji wa timu pinzani ama mwamuzi wa mchezo ni kosa ambalo litamfanya mchezaji aliyefanya kitendo hiko kuzawadiwa kadi nyekundu ama ya njano, hiyo ikiwa ni moja ya tahadhari ya kujikinga na Janga la virusi vya corona,

Katika taarifa ambayo ilitolewa na FA, ilieleza kuwa kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa sheria ya 12, ambayo inaeleza kuwa matumizi ya lugha chafu au ishara ya kuashiria matusi kwa mwingine wakati mchezo unaendelea ni kosa kisheria na adhabu yake ni kadi nyekundu ama ya njano.

Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa ikiwa Mwamuzi ataona kuwa hakukuwa na makusudio ya tukio hilo anapaswa kutoa onyo kali na ikiwa mchezaji huyo atarudia tena amtoe nje kwa kadi nyekundu.

Aidha taarifa hiyo imeisisitiza kuwa waamuzi wawe macho na wachezaji ambao wamekuwa na tabia ya kutema mate Uwanjani kwa kuongea nao na kuwakataza kufanya jambo hilo kwa usalama wao na wachezaji wenzao ingawa kufanya hivyo sio kinyume cha sheria.

Nchini England kumekuwa na lundo kubwa la watu ambao wamefungwa Gerezani kwa kosa hilo la kukohoa mbele ya wananchi wenzao.

Pia Machi mwaka huu, Straika wa Atletico / Madrid, Diego Costa alilaaniwa vikali na klabu yake baada ya kumkohelea muandishi wa habari wakati wa mkutano nao baada ya mchezo wao wa Klabu Bingwa barani Ulaya dhidi ya Liverpool


Comments