NYOTA MMOJA BARCELONA ANA CORONA
Kikosi cha timu ya soka ya Barcelona ya Hispania BARCELONA, Hispania Barcelona imesema kuna mchezaji mmoja amebainika kuwa na ugonjwa wa Covid 19. Mchezaji huyo ambaye jina lake limefichwa, ni miongoni mwa wachezaji 9 walioripoti katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya na tayari amejiweka karantini nyumbani kwake huku akiwa hana dalili yoyote ya kuumwa. Barcelona imesema hajasogeleana na mchezaji yoyote ambaye atasafiri kwenda Ureno kucheza mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Tayari Valencia ilithibitisha visa viwili vya corona wiki hii huku Atletico Madrid ikiripoti watu wawili kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Barcelona itakipiga na Bayern Munich Ijumaa katika mechi ya robo fainali huku Atletico na RB Leipzig wakitangulia kesho.