Posts

NYOTA MMOJA BARCELONA ANA CORONA

Image
  Kikosi cha timu ya soka ya Barcelona ya Hispania BARCELONA, Hispania Barcelona imesema kuna mchezaji mmoja amebainika kuwa na ugonjwa wa Covid 19. Mchezaji huyo ambaye jina lake limefichwa, ni miongoni mwa wachezaji 9 walioripoti katika kambi ya maandalizi ya msimu mpya na tayari amejiweka karantini nyumbani kwake huku akiwa hana dalili yoyote ya kuumwa. Barcelona imesema hajasogeleana na mchezaji yoyote ambaye atasafiri kwenda Ureno kucheza mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Tayari Valencia ilithibitisha visa viwili vya corona wiki hii huku Atletico Madrid ikiripoti watu wawili kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Barcelona itakipiga na Bayern Munich Ijumaa katika mechi ya robo fainali huku Atletico na RB Leipzig wakitangulia kesho.

MORRISON ASHINDA KESI

Image
  Winga wa Simba, Benard Morrison Na Arone Mpanduka,  DAR ES SALAAM KIUNGO wa Yanga,  Bernard Morrison raia wa Ghana leo Agosti 12 ameshinda shauri lake dhidi ya Yanga ambalo lilikuwa ni kuhusu mkanganyiko wa mkataba wake ndani ya klabu hiyo. Morrison alikuwa akisema kuwa mkataba wake ni wa miezi sita na umekwisha muda wake huku Yanga ikieleza kuwa alisaini dili lingine la miaka miwili. Baada ya kesi hiyo kuskilizwa kwa muda wa siku tatu mfululizo tangu, Agosti 10,11 na 12 leo shauri limetolewa rasmi makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF). Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, Elias Mwanjala, amesema mkataba wa Yanga na Morrison, una mapungufu makubwa upande wa Yanga na wamempa faida Morrison. . "Tumekuwa makini katika kufuata haki na kamati yetu ilikuwa makini, kulikuwa na mapungufu makubwa upande wa tarehe ambapo kuna sehemu ilionyesha kuwa amesaini Machi 20 na nyingine ikionyesha tarehe tofauti. "Pia kuna ukurasa wa saini kwenye mkataba...

SAMATTA, ALI KIBA WATUNISHIANA MISULI

Image
Na Arone Mpanduka, DAR ES SALAAM Msanii Ali Kiba pamoja na mshambuliaji wa Aston Villa ya Uingereza Mbwana Samatta wametunishiana misuli kuelekea mchezo maalum wa hisani utakaopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mechi hiyo ambayo imeandaliwa na Taasisi ya SamaKiba, huchezwa kila mwaka kwa lengo kusaidia watu wenye uhitaji hasa wanafunzi ambapo Samatta huunda timu iitwayo Team Samatta huku Ali Kiba akiunda timu iitwayo Team Kiba. Ali Kiba ambaye kikosi chake mwaka jana kilifungwa mabao 6-3, amesema safari hii hatokubali kunyanyaswa huku Samatta akiahidi kuendeleza rekodi ya kichapo kwa wapinzani wao. Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara, ambaye ni Ofisa Habari wa Klabu ya Simba. “Nina kikosi changu ambacho ninaamini kitafanya vizuri siku hiyo.Nitaendeleza ubabe wa kumchapa nyingi bwana Kiba.”alisema Samatta. Kwa upande wa Kiba yeye kamtaja...

UKIMKOHOLEA MWENZIO TU, KADI

Image
Wachezaji wakileteana ubabe uwanjani LONDON, England Wakati msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12, mwaka huu chama cha soka nchini humo kimeandaa kanuni mpya ambayo itaanza kutumika katika msimu ujao. Kanuni hiyo inaeleza kuwa ikiwa mchezaji wa timu moja atamkoholea mchezaji wa timu pinzani ama mwamuzi wa mchezo ni kosa ambalo litamfanya mchezaji aliyefanya kitendo hiko kuzawadiwa kadi nyekundu ama ya njano, hiyo ikiwa ni moja ya tahadhari ya kujikinga na Janga la virusi vya corona, Katika taarifa ambayo ilitolewa na FA, ilieleza kuwa kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa sheria ya 12, ambayo inaeleza kuwa matumizi ya lugha chafu au ishara ya kuashiria matusi kwa mwingine wakati mchezo unaendelea ni kosa kisheria na adhabu yake ni kadi nyekundu ama ya njano. Pia taarifa hiyo ilieleza kuwa ikiwa Mwamuzi ataona kuwa hakukuwa na makusudio ya tukio hilo anapaswa kutoa onyo kali na ikiwa mchezaji huyo atarudia tena amtoe nje kwa kadi nyekundu. Aidha taarifa hiy...

WILLIAN HUYOO ARSENAL

Image
Winga wa Chelsea Willian London, ENGLAND Arsenal imetajwa kuongoza mbio za kumuwania winga wa Chelsea, Willian baada ya nyota huyo raia wa Brazil kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na klabu yake. Taarifa iliyotolewa na mtandao wa The Sun, imefichua kuwa mazungumzo baina ya wawakilishi wa Arsenal na wale wa mchezaji huo yako katika hatua za mwisho ambapo Willian mwenye umri wa miaka 31 atajiunga nao akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika msimu huu. Chelsea ilikuwa inapanga kumuongezea mkataba wa miaka mwili, nyota huyo huku yeye akihitaji uwe na urefu wa miaka mitatu jambo ambalo wameshindwa kufikia muafaka na kupelekea Willian aamue rasmi kufungasha virago na kusaka malisho mazuri zaidi. Klabu takribani tano zimetajwa kuingia katika vita ya kumuwania Willian lakini ni Arsenal ambayo kwa mujibu wa taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wameshafikia muafaka na kilichobakia ni mchezaji huyo kusaini mkataba wa mia...

MORRISON 'ATUA' SPUTANZA

Image
Winga wa Yanga Benard Morrison Na Arone Mpanduka, DAR ES SALAAM Chama cha wachezaji wa soka nchini (SPUTANZA) kimezipokea taarifa za utovu wa nidhamu za winga wa Yanga Benard Morrison kwa masikitiko makubwa na kusema kwamba mchezaji huyo amejishushia hadhi yake. Julai 12 mwaka huu, winga huyo mwenye uraia wa Ghana aliondoka uwanjani moja kwa moja wakati mchezo wa watani wa jadi ukiendelea wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA. Morrison aliondoka uwanjani kinyume na utaratibu baada ya kufanyiwa mabadiliko na kocha Luc Eymael, kwani alipaswa kwenda kuketi katika benchi la wachezaji wa akiba lakini yeye alilipita benchi hilo na kisha kwenda kubadilisha nguo kwenye vyumba vya kupumzikia na kuondoka zake. Akizungumza na Mchakamchaka hivi karibuni Mwenyekiti wa SPUTANZA Musa Kisoki alisema kwa mujibu wa kanuni mchezaji huyo hakupaswa kuondoka wakati mechi ikiwa inaendelea kwani alikuwa akihesabika kama sehemu ya mchezo. “Mchezaji unapokuwa katika benchi la wachezaji wa akiba un...

BANCE ASTAAFU KUICHEZEA TIMU YA TAIFA

Image
OUAGADOUGOU, Burkinafaso Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burkinafaso Aristide Bance ,35, ametangaza rasmi kustaafu kucheza timu ya taifa baada ya miaka 17 toka alipoanza kuichezea 2003. Bance ambaye amecheza soka katika mataifa mbalimbali ya Asia, Afrika na Ulaya sasa ataendelea kuitumikia timu yake ya Horoya AC ya Guinea pekee. Bance ameichezea Burkinafaso michezo 73 na kufunga magoli 22, alikuwa sehemu ya kikosi cha Burkinafaso kilichoshiriki michuano ya AFCON 2013, 2015 na 2017. Mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ilikuwa Novemba 2017 katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Cape Verde katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018.