WILLIAN HUYOO ARSENAL
Winga wa Chelsea Willian London, ENGLAND Arsenal imetajwa kuongoza mbio za kumuwania winga wa Chelsea, Willian baada ya nyota huyo raia wa Brazil kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na klabu yake. Taarifa iliyotolewa na mtandao wa The Sun, imefichua kuwa mazungumzo baina ya wawakilishi wa Arsenal na wale wa mchezaji huo yako katika hatua za mwisho ambapo Willian mwenye umri wa miaka 31 atajiunga nao akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Chelsea kumalizika msimu huu. Chelsea ilikuwa inapanga kumuongezea mkataba wa miaka mwili, nyota huyo huku yeye akihitaji uwe na urefu wa miaka mitatu jambo ambalo wameshindwa kufikia muafaka na kupelekea Willian aamue rasmi kufungasha virago na kusaka malisho mazuri zaidi. Klabu takribani tano zimetajwa kuingia katika vita ya kumuwania Willian lakini ni Arsenal ambayo kwa mujibu wa taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kuwa wameshafikia muafaka na kilichobakia ni mchezaji huyo kusaini mkataba wa mia...